Hıdrellez ni moja ya sikukuu za msimu Mei 6 katika kalenda ya Gregory kusherehekea kuwasili kwa msimu wa spring. Baada ya msimu wa baridi katika Anatolia, siku ya kuonyesha matarajio ya kuingia msimu wa hali ya hewa mpya(Spring) husherehekewa kila Mei 6 na huitwa Hıdırellez.
Khidr na Eliya manabii wanaaminika kukutana katika tarehe hii duniani. Hidirellez, Uturuki siku hii husherehekewa na waislamu pamoja na wakristo katika maeneo mengi kama njia ya kuukaribisha mwaka mpya.
Siku kabla ya Hıdrellez,nyumba husafishwa na vyakula tofauti hupikwa nam ara nyingi watu hupenda kwenda kutembelea mahala penye miti mengi kwa ajili ya kusherehekea.
Wakati mwingine moto huwashwa na watu huomba dua .Watu huandika kila watakacho katika mti wa uaridi na matakwa yao husomwa kabla ya jua kuzama.
Wakati mwingine matakwa hayo hurushwa motoni au baharini ili yaweze kuwa kweli.
Mwaka 2016 Macedonia na Uturuki zilishereheeka kwa pamoja kuja kwa msimu wa SPRING na 2017siku hiyo ya Hidirellez ikaorodheshwa na UNESCO katika kumbukumbu za ubinadamu duniani.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇