May 20, 2019

SHAMHUNA AFARIKI DUNIA MJINI ZANZIBAR

Zanzibar, Tanzania
ALIYEKUWA Naibu waziri kiongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ali Juma Shamhuna (pichani), amefariki Dunia.

Taarifa zilizothibishwa zinasema Shamhuna amefariki usiku wa kuamkia leo, ingawa taarifa za kifo hicho zilianza kusambaa jana jioni mjini Ugunja kisiwani Zanzibar.

Katika enzi za uhai wake Shamhuna ambaye ni Kiongozi mwandamizi ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi serikalini kwa awamu tofauti. 

Amewahi kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa serikali ya Zanzibar na Waziri wa Maji, Ardhi, Nyumba na Nishati,
Taarifa zinasema, inatarajiwa Shamhuna atazikwa leo Mei 20, 2019, mjini Unguja, Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages