LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 3, 2019

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA MAWAKILI TANGANTIKA (TLS)

Rais wa TLS Dk. Rugemeleza Nshala akimkabidhi Mwanasheria Mkuu wa Serikali  shajala za TLS mara baada ya mazugumzo yao yaliyowajumuisha pia wajumbe wa Baraza la  Uongozi la TLS. Picha zaidi/ BOFYA HAPA

Na Mwandishi Maalum, Dodoma

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi,  amesema, Serikali inatambua mchango wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika ( TLS) katika  kuimarisha na kudumisha Utawala wa Sheria  nchini.

Amesema  wakati wote  Serikali ipo tayari kupokea maoni na ushauri kutoka TLS ilimradi kwamba,  maoni  au ushauri huo unajikita katika  kujenga, kuimarisha, hauegemei upande wowote, wenye staha na  usio na mashinikizo.

“ Kwanza niwashukuru sana kwa kuja kukutana  na kufanya  mazungumzo nami, niwapongeze wewe Rais kwa kuchaguliwa  kuwa Rais wa TLS pamoja  na  wote  mliochaguliwa katika baraza la uongozi.  Ni matumaini yangu kwamba, hamtawaangusha  wanachama wenu waliowachagua, msiwaagushe tafadhali”  Akasema  Mwanasheria Mkuu wa Serikali  na  kuongeza

“Wakati wote Serikali  imekuwa ikithamini sana mchango wenu na maoni yenu. Na kwa kweli mmekuwa mkitoa mchango  na maoni mazuri sana, niwahakikishe kwamba Serikali  wakati wote ipo  tayari kushirikiana nanyi. Jambo la muhimu ni  kuwa na  majadiliano ( dialogue) pale ambapo  mnaona    kunajambo la kujadiliana kabla ya  kulitolea   matamko.

“Niwahakikishe kwamba, Serikali kwa ujumla na hasa Rais John Pombe Magufuli  katika   uongozi wake anapenda sana Sheria na anataka  mambo yafanyike kisheria na kwa kuzingatia sheria ” akasisitiza Profesa Kilangi

Profesa Kilangi ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumza na  ujumbe wa  Balaza la Uongozi la TLS  likiongozwa na Rais wake Dk. Rugemeleza Nshala.
Mazungumzo  kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na  Ujumbe wa Balaza la  Uongozi yaliyochukua zaidi ya  masaa matatu, yalifanyika siku ya Alhamisi katika  ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mitumba- Ihumwa  Jijini Dodoma.

“Niwaombe sana katika uongozi wenu msimamie sana  weledi  wa tasnia ya Sheria, hili nawaomba sana, sisi sote ni  maofisa wa Mahakama, ni katika mkutadha huu tunatakiwa kutekeleza  majukumu yetu ya  uofisa Mahakama kwa welidi wa hali ya juu  sana  na kwa kuzingiatia misingi  na maadili ya kazi zetu. Lisimamieni sana hili, simamie professionalism” akasisitiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Rais wa TLS Dk, Rugemeleza  Nshala  pamoja na kumshukuru   Mwanasheria Mkuu wa  Serikali kwa kuwakubalia ombi lao  na kukutana nao. Alisema kuna  mambo kadhaa ambayo walitamani au waliona ni vema   wakabilishana   naye mawazo.

Dk Nshala aliyataja baadhi ya   mambo hayo kuwa ni  pamoja na kuangalia namna bora itakayowawezesha TLS na   wadau wengine wa  Sheria nchini, akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya  kushirikiana  katika kuhakikisha kwamba  Mawakili wa kujitegemea na Mawakili wa Serikali wanatekeleza majukumu yao kwa weledi na kwa kuzingatia maadili na miiko ya  kazi zao.

Jambo jingine ambalo Dk. Nshala   kwa niaba ya jumbe wake aliliwasilisha kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali  ni  la namna ya kuangalia  jinsi ya kuifanyia marekebisho baadhi ya  vifungu vya Sheria  ya  TLS hasa katika kifungu cha uchaguzi wa Viongozi  unaotakiwa   kufanyika  kila mwaka.

“Katika  mkutano wetu wa Arusha wanachama tulilijadili hili la uchaguzi wa kila mwaka, ni hitajio la kisheria lakini gharama za kukutana kila mwaka ni kubwa sana  na zinabebwa na wanachama, hivyo tulijadiliana kuona  namna gani tunaweza kuliboresha hili kwa kujadiliana na wadau wengine na kwa kuangalia mifano ya nchi nyingne akasema “ Rais wa TLS.

Dk. Nshala  pia alizungumzia kuhusu mitaala ya  mafunzo  Sheria katika  Vyuo Vikuu na kushauri kwamba  wadau wa Sheria wanapashwa kukaa na kujadiliana namna bora ya  kuuboresha  ili iendane na wakati.

Kwa mujibu wa  Rais huyo wa TLS  amesema kwa uzoefu wake na katika  utekelezaji wa majukumu  yake kuna mifano hai  ya mapungufu ya kiutendaji  kwa kwa baadhi  ya mawakili  ambayo mengi  kati   ya hayo  ni  ukosefu wa mafunzo Stahiki

Katika hilo  la  uboreshaji wa mfumo wa ufundishaji, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema anakubaliana nalo kwa asilimia kubwa, na kwamba , tatizo ambalo  yeye analiona ndiyo changamoto kubwa katika tasnia ya Sheria ni mafunzo  kwa vitendo.

Mwanasheria Mkuu wa  Serikali Profesa Kilangi na  Uongozi wa TLS walijadili pia kuhusu namna bora ya  kuhakikisha kwamba  Sheria zinazofanyiwa urekebu  na  mara zikisha pitishwa na  Bunge Ofisi ya Mwanasheria Mkuu isisambaze  ili zinawafikia wadau  kwa wakati.

Vile vile walibadilishana  mawazo kuhusu  haja na umuhimu wa  kuzifanyia urekebu  baadhi ya Sheria ambazo zinamatatizo   au changamoto katika utekelezaji wake.  Baadhi  ya Sheria hizo ni  pamoja na baadhi ya vifungu vya Sheria ya Jinai na  Sheria ya Usuluhishi wa migogoro nje ya Mahakama.

Walibadilishana mawazo pia kuhusu mazingira ya utendaji  kazi wa Mawakili hasa mawakili wa kujitegemea ambao  Dk. Nshala alisema   wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazopashwa kutafutiwa ufumbuzi.
Mkutano huo pia ulihudhuriwa na  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Dk. Evaristo Longopa na  Mkurugenzi wa Idara ya  Uratibu na  Utoaji wa Huduma Dk. Gift Kweka.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Dodoma
3/5/2019

4 comments:

  1. Simply wish to say your article is as surprising.
    The clearness in your post is just nice and i could assume you are an expert on this subject.
    Fine with your permission let me to grab your feed to keep up to date
    with forthcoming post. Thanks a million and please carry on the gratifying work.

    ReplyDelete
  2. I truly love your blog.. Excellent colors & theme. Did you develop this web site yourself?
    Please reply back as I'm attempting to create my very
    own site and would love to learn where you got this from or just what the theme is named.
    Many thanks!

    ReplyDelete
  3. Oh my goodness! Amazing article dude! Thank you, However I am
    having difficulties with your RSS. I don't know the reason why I am unable to subscribe to it.
    Is there anyone else getting identical RSS issues? Anyone that knows
    the solution will you kindly respond? Thanx!!

    ReplyDelete
  4. I read this article fully about the difference of most up-to-date and
    earlier technologies, it's awesome article.

    ReplyDelete

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages