LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 8, 2019

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA BUNGE LA AFRIKA

Makamu wa kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika. Stephen Masele akimpokea Rais Mstaafu wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete alipotembelea Makao Makuu ya Bunge la Afrika “Pan- African Parliament” yaliyopo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, Mei 7, 2019

Na Kadama Malunde, Johannesburg
Rais Mstaafu wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete ametembelea Makao Makuu ya Bunge la Afrika “Pan- African Parliament” yaliyopo Jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.


Dk. Kikwete ambaye ni Kiongozi wa Timu ya Waangalizi wa Umoja wa Afrika wa Uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini mwaka 2019 amepokelewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele leo Jumanne Mei 7,2019.

Amelipongeza Bunge la Afrika kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kusimamia Demokrasia, Utawala na Masuala ya Ulinzi na Usalama barani Afrika.

“Mimi nilikuwa miongoni mwa Mawaziri wa Mambo ya Nje ambao tulikutana kule Sirte Libya kuandaa kanuni za kuanzishwa kwa Bunge la Afrika,hivyo ninayo furaha kubwa kuona hatua kubwa ya maendeleo ya bunge, Nawapongeza sana Rais na Makamu wa Rais kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuendeleza bunge hili na Waafrika wote tunawatagemea”, amesema Dkt. Kikwete

“Leo na timu yangu ya uangalizi ambao tupo hapa Afrika Kusini kwa ajili ya uangalizi wa Uchaguzi mkuu wa mwaka huu,na ninashukuru miongoni mwa timu yangu wabunge wa bunge la Afrika ni miongoni mwa wajumbe wangu,nawapongeza sana Bunge la Afrika kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika kusimamia demokrasia”, ameongeza Dkt. Kikwete.

Kwa upande, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mheshimiwa Stephen Masele amemshukuru na kumpongeza, Mheshimiwa Kikwete kwa mchango wake mkubwa kwa bara la Afrika kwenye nyanja za afya,elimu na demokrasia.

"Sisi viongozi vijana tuna mengi ya kujifunza kutokana na uzoefu wako mkubwa kwenye masuala ya uongozi na siasa za kimataifa, binafsi nakushukuru sana kwa malezi yako  ambapo kwa uwezo wa mwenyezi Mungu nimeweza kufika hapa nilipo kiuongozi", amesema Masele.

Aidha amemuahidi Mheshimiwa Kikwete kuwa Bunge la Afrika litatoa ushirikiano wote unaohitajika ili kuweza kutimiza majukumu yake katika uangalizi wa uchaguzi Mkuu wa Afrika Kusini mwaka 2019.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages