LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 12, 2019

POLEPOLE AWATAKA VIJANA KUINGIA KATIKA MAPAMBANO YA KUIKOMBOA AFRIKA KIUCHUMI.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole ambaye pia ni mlezi wa Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM, akizungumza na wahitimu wakati wa mahafali ya saba ya  Wanafunzi wa vyuo hivyo, yaliyofanyikia jana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha zaidi za Mahafali hayo BOFYA HAPA
----------------------------
Na Bashir Nkoromo
Vijana wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika mapambano ya vita vya ukombozi wa kiuchumi Barani Afrika, badala ya vita vya kudai uhuru ambavyo vilikwishakamilishwa na waasisi wa nchi za bara hilo akiwemo Baba wa taifa Mwalimu Nyerere kwa upande wa Tanzania.

Mwito huo umetolewa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole katika mahafali ya saba ya Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu wa Umojua wa Vijana wa CCM, yaliyofanyika jana katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

"Mwanzoni kabisa bara la Afrika lilikuwa na kiu kubwa na kuhakikisha nchi ndani ya bara hili zinajitawala kisiasa, sasa kazi hii ikafanywa na na kukamilishwa kabisha na Baba wa Taifa mwalimu Nyerere na Wenzake kama kina Osagyefo Kwame Nkrumah (Ghana), Samora Machel (Msumbiji), Keneth Kaunda (Zambia), Jose Eduardo Dos Santos (Angola), Samu Nojoma (Namibia) na Nelson Mandela (Afrika Kusini), kwa hiyo vita iliyopo mbele ya kizazi hiki ni ya mapambano ya kulikomboa bara la Afrika kiuchumi", alisema Polepole.

Alisema, kwa upande wa Tanzania mapambano hayo yanaongozwa kwa dhati kabisa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli na dhamira ya kufikia mafanikio inaonekana wazi, kwa hiyo jukumu walilonalo Watanzania hasa Vijana ni kumuunga mkono kwa kutumia nguvu, elimu na maarifa katika mapambano hayo.

Polepole aliwataka vijana hasa wasomi kutumia elimu zao kutoa ufafanuzi katikia nyanja mbalimbali pale wanapoona kuwa kuna maadui wanajaribu kupotosha juhudi za Rais Dk. Magufuli katika kuinua uchumi wa Tanzania kupitia ujenzi wa miradi mbalimballi.

Mapema Katibu wa Seneti mkoa wa Dar es Salaam, Erick Kibada alisema, katika mahafali hayo wahitimu kutoka vyuo 30 vikiwemo vyuo na vyuo vikuu wameshiriki mahafali hayo na kuwaataka kuendelea kuwa makada wa CCM hata baada ya kumaliza masomo yao. 

Mahafali hayo nalinogeshwa na waalikwa mbalimbali wakiwemo wasanii wa Muziki wa kizazi kipya, Raivan na  Zuwena Mohammed almaarufu kwa jina la Shilole au Shesh Baby.

Wasanii hao walitumia fursa hiyo kuwapa nasaha mbalimbali wahitimu ikiwa ni pamoja na kuwataka kiloa mmoja wao kusaka vipaji walivyo navyo na kuivitumia ili elimu zao ziwe nyenzo ya kuvifanya vipaji vyao kuwa vyenye manufaa zaidi.

Pia kwa nyakati tofauti wasanii hao waliwashauri wahitimu kuwa na bidii, nidhamu na kumtanguliza Mungu ili kupata mafanikio katika kila watakalofanya kwa ajili ya kujitafutia maendeleo.⇰ PICHA KEM KEM ZA MAHAFALI HAYO/BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages