Takriban magaidi 20 wa YPG / PKK wameuawa katika mlipuko mabomu mawili huko Syria.
Kwa mujibu wa habari,milipuko ilikuwa imelenga makao makuu ya usalama na kijeshi yanayohusiana na kundi la kigaidi la YPG / PKK katika jimbo la kaskazini la Raqqah la Syria siku ya Jumamosi.
Vyanzo vya habari vinasema kuwa inawezekana mlipuko huo umesababishwa na magari yaliyokuwa yametegwa na mabomu.
Hakujakuwa na kundi lolote lililotangaza kuhusika na mashambulizi hayo.
Magaidi ya YPG / PKK wameweka cordon ya usalama karibu na maeneo ya mashambulizi.
Siku ya Jumamosi, magaidi watano wa YPG / PKK waliuawa katika mabomu yanayodaiwa kulipuliwa na kundi la kigaidi la Daesh huko Manbij.
Magaidi YPG / PKK wamekuwa na udhibiti wa Raqqah tangu Oktoba 2017.
Kundi la PKK linatambuliwa kama kundi la kigaidi na Umoja wa Ulaya,Umoja wa Mataifa na Uturuki.
Ahaa, its pleasant discussion about this post here at this
ReplyDeletewebsite, I have read all that, so at this time me also commenting here.