LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 13, 2019

GADI YA PWANI LIBYA YAWAOKOA WAHAMIAJI HARAMU 150

Kwa mujibu wa msemaji wa gadi hiyo, Ayoub Gassim, kati ya waliookolewa ni pamoja na wanawake 16 na watoto wanne kwenye boti iliyokuwa na wahamiaji wapatao 96.
Msemaji huyo ameeleza kuwa watu hao waliokolewa katika mji wa Zawiya, kilometa 50 magharibi mwa Tripoli.
Amesema, wamepatiwa misaada na kupelekwa katika kambi za wakimbizi. Gassim ameongeza kuwa kando ya wahamiaji hao, boti nyingine iliyobeba wahamiaji 51 ilizuiwa katika mji wa Khomos kilomita 120 mashariki mwa Tripoli.
Hayo yanaripotiwa siku moja baada ya serikali ya nchi jirani ya Tunisia kutangaza kuwa wahajiri 70 waliaga dunia katika ajali ya Ijumaa katika pwani ya Tunisia.
Wahajiri haramu wakielekea Ulaya
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) lilitangaza kuwa zaidi ya wahajiri elfu mbili waliaga dunia katika bahari ya Mediterania katika mwaka uliopita wa 2018.
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhajiri IOM, njia ya majini ya kutoka Libya kuelekea nchi za Ulaya ikiwemo Italia na Malta, ndiyo njia hatari zaidi kwa maafa ya roho za watu inayotumiwa na wahajiri haramu kutoka nchi hasa za Kiafrika kwa safari za kuelekea barani Ulaya kwa lengo la kutafuta maisha mazuri.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages