Baadhi ya Wananchi wakihudhuria futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, nyumbani kwake Kibele Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohameed Shein, akijumuika na Wananchi wa Kijiji cha Kibele Wilaya ya Kati Unguja katika futari iliofanyika nyumbani kwake Kibele Unguja, kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis na kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia Dua, ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleoh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya futari iliofanyika Kibele Wilaya ya Kati Unguja, kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum Mhe. Soud Said Soud, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliofanyika nyumbani kwake Kibele Wilaya ya Kati Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsalimia Mtoto Sleyum Khamis mkaazi wa Kibele Wilaya ya Kati Unguja, baada ya kumalizikwa kwa Futari aaliuowaandalia Wananchi wa Kibele iliofanyika nyumbani kwake Kibele Mkoa wa Kusini Unguja. (PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR).
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇