MWENYEKITI Mtendaji wa Kampuni za IPP Dk. Reginald Mengi, amefariki dunia usiku wa kumakia leo Mei 2, 2019.
Taarifa zinasema Dk. Mengi (Pichani) amefariki dunia akiwa Dubai Falme za Kiarabu.
Hata hivyo taarifa vituo vilivyotangaza taarifa hiyo vya Radio One na ITV vya IPP, havikutoa ufafanuzi zaidi kuhusu chanzo cha kifo hicho.
Dk. Reginald Abraham Mengi alizaliwa Wilayani Machame Mkoani Kilimanjaro ambako mara nyingi alikaririwa akisema amezaliwa kwenye familia masikini.
Lakini pamoja na kuwa kwenye mazingira kama hayo, Dk. Mengi hakukata tama na ndoto yake ya kufanikiwa kimaisha ilimpelekea kusoma kwa bidii ambapo alifanikiwa kusomea masuala ya uhasibu nchini Uingereza.
Baada ya kufanikiwa kumaliza masomo yake alirejea nyumbani mnamo mwaka 1971 na kuajiriwa na Kampuni ya Uhasibu na Ukaguzi wa mahesabu ya Coopers & Lybrand Tanzania (kwa sasa inajulikana kama PriceWaterHouseCoopers) hadi Septemba 1989 na katika kipindi hicho alichaguliwa kuwa mwenyekiti na Kiongozi mwenza.
Mnamo Oktoba 1989 Dk. Mengi aliondoka Coopers & Lybrand Tanzania na kujielekeza kwenye biashara zake binafsi na kuanzisha IPP Limited, ambayo ilikuja kuwa kampuni kubwa kabisa ya kibinafsi nchini Tanzania.
Biashara ambazo Watanzania wa kawaida walizifahamu, ni pamoja na kumiliki vyombo vya habari mashuhuri kabisa hapa nchini ITV/Radio One, Kampuni ya magazeti ya The Guardian Limited lakini pia Dkt. Mengi chini ya kampuni yake ya IPP alikuwa akifanya biashara mbalimbali na hivi karibuni alisaini kandarasi ya kuanzisha kiwanda cha kutengeneza magari hapa hapa nchini, lakni pia kiwanda cha kutengeneza madawa ya binadamu na vingine vingi.
Your Ad Spot
May 2, 2019
DK. REGINALD MENGI AFARIKI DUNIA AKIWA DUBAI
Tags
featured#
KIJAMII#
Share This
About Bashir Nkoromo
KIJAMII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇