LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 10, 2019

WHO; WAKIMBIZI WA NDANI ETHIOPIA WANAKARIBIA MILIONI 1

Kwa mujibu wa taarifa ya WHO, ripoti ya serikali inasema takribani watu 995,559 walifurushwa na mapigano ya makabila katika maeneo ya Gedeo na magharibi mwa Guji mnamo mwezi Februari na Machi mwaka huu ambapo serikali imetoa wito katikati ya mwezi uliopita kwa wadau Ili kuweza kukabiliana na hali inayoshuhudiwa.
WHO imewasilisha vifaa tiba kwa ajili ya matibabu ya watu 115,000 kwa muda wa miezi mitatu pamoja na mifuko yenye vifaa tiba ikiwemo, glovu, sindano na dawa kwa ajili ya matibabu ya watu 70,000 kwa tiba ya miezi mitatu. Aidha WHO imetoa tiba kwa ajili ya watoto 250 walio na utapiamlo uliokithiri kwa kipindi cha miezi mitatu.
WHO imesema hali ya kibinadamu inayoshuhudiwa ni ngumu ambapo shirika hilo limeimarisha nguvu kazi na kupanua vituo vya afya kwa ajili ya kukabiliana na wagonjwa.
Shirika hilo limesema itashirikiana na wizara ya afya, mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine kwa ajili ya kuimarisha huduma za misaada ikiwemo maji, huduma za kujisafi na kujisafi na kampeni za chanjo.
Serikali ya Ethiopia kwa upande wake imepeleka wataalam 117 wa afya ikiwemo madaktari, wahudumu wa afya kwa ajili ya kujaza pengo la wahudumu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages