LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 14, 2019

WATU WAZIDI KUPOTEZA MAISHA KATIKA MAFURIKO IRANI

Watu wazidi kupoteza maisha katika mafuriko Iran

Mkurugenzi wa Taasisi ya Madawa nchini Iran, Ahmed Shujai, amrsema kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha yao kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa imeongezeka hadi 76 katika majimbo 25 ya 31.
Shujai, ameviambia vyombo vya habari vya Iran  kuwa athari ya mafuriko katika majimbo tofauti ni kama ifuatavyo alisema Loristan 14, Gulistan 8, Mazenderan, Hemedan na Khuzestan 5, Kaskazini Khorasan na Kohgiluye-Buyer 3, Ilam 2, Khorasani Rezevi, Simnan, Kirmanshah, Kum, Isfahan, Kazvin na Zencan watu 76 wamepoteza maisha.
Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa katika mikoa 25 ya Iran tangu Machi 17 yamesababisha uharibifu mkubwa na vifo.
Shirika la Turk Kizilay, ambayo imechukua hatua kusaidia waathiirika nchini Iran imekuwa ikisaidiana na shirika la msalaba mwekundu kutoa misaada nchini humo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages