LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 14, 2019

121 WAUAWA LIBYA KATIKA MAPIGANO


Mashirika ya afya ya Umoja wa Mataifa yamesema mapigano yanayoendelea nchini Libya kati ya makundi hasimu ya wanamgambo yanayogombania udhibiti wa mji mkuu wa Tripoli yamesababisha vifo vya takriban watu 121.

Shirika la Afya Duniani WHO limesema leo hii kwamba watu wapatao 561 wamejeruhiwa tangu mashambulizi makubwa ya jeshi la kibinafsi LNA linaloongozwa na Khalifa Haftar yalipoanza Aprili 5.

Umoja wa Mataifa umesema mapema wiki hii kwamba watu zaidi ya 8,000 wamepoteza makaazi yao kutokanana mapigano hayo.

Machafuko hayo yanatishia kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe kama vile vya mwaka 2011 ambavyo vilipelekea kuondoshwa madarakani na kuuawa kwa kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Moammar Gadhafi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages