LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 15, 2019

UNICEF: WATOTO MILINI 1.5 WANAHITAJI MSAADA KUSINI MWA AFRIKA KUFUATIA KIMBUNGA IDAI

Akizungumza kuhusu hali ya watoto baada ya kimbunga hicho mkurugenzi mkuu wa UNICEF, Henrietta Fore ambaye alizuru Msumbiji pindi tu baada ya kutokea kimbunga hicho hususan katika mji wa Beira amesema, “watoto wanaoishi katika makazi yaliyojaa watu mbali na makazi yao wako hatarini ya magonjwa, kutumikishwa na ukatili.”
UNICEF imesema watoto milioni moja nchini Msumbiji, 443,000 nchini Malawi na 130,000 nchini Zimbabwe wana mahitaji makubwa ikiwemo huduma ya afya, lishe, elimu na maji.
Tangu kimbunga hicho kupiga Msumbiji mwezi mmoja uliopita visa vya kipindupindu vimeongezeka kufikia hadi 4,600 huku visa vya malaria vikifika 7,500.
UNICEF imesema kusitishwa kwa huduma muhimu huenda kukasababisha mlipuko wa magonjwa na ongezeko la utapiamlo ambapo watoto wako hatarini.
Kwa mantiki hiyo Bi. Fore amesema, “barabara kuelekea kupona, itakuwa ndefu na ni muhimu kwa washikadau wa misaada ya kibinadamu wahusike katika kila hatua.”
Kwa mujibu wa UNICEF, takriban nyumba 200,000 ziliharibiwa nchini Msumbiji tu na kwa sababu kimbunga hicho kilitokea wiki chache tu kabla ya mavuno, uhakika wa chakula uko njia panda.
Wakati huo huo, maelfu ya watu wanasalia katika kambi za muda mfupi ambapo UNICEF imeelezea wasiwasi wake kuhusu hatma ya watoto takriban 130,000 waliolazimika kuhama nchini Musumbiji na Malawi.
UNICEF imesisitiza umuhimu wa kusaidia watoto na familia kukabiliana na hali ya sasa na kurejelea katika maisha yao hapo baadaye.
UNICEF imetoa ombi la dola milioni 122 kwa ajili ya kusaidi watoto na familia walioathirika na kimbunga na athari zake nchini Msumbiji, Zimbabwe na Malawi kwa kipindi cha miezi tisa ijayo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages