LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 12, 2019

UMOJA WA MATAIFA WAITAKA SUDAN KUSHIRIKIANA NA ICC

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Haki za Binadamu imeitaka serikali ya mpito ya Sudan kushrikiana na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ya (ICC) ambayo ilitoa hati ya kukamatwa kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Oma al Bashir.

Omar al Bashir aling’olewa madarakani kwenye mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea Alhamisi baada ya kuiongoza nchi hiyo tangu mwaka 1989 baada ya kutwaa madaraka kwa mapinduzi ya kijeshi.

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) ilitoa hati ya kukamatwa kwa al Bashiri miaka 15 iliyopita lakini tangu wakati huo hakuna lililokuwa limefanikiwa.

Hata hivyo tayari serikali ya mpito ya nchi hiyo imeshatangaza kuwa al Bashir atashtakiwa kwa sheria za ndani ingawa kauli hiyo haikubainisha iwapo nchi hiyo inapingana na mahakama hiyo ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages