LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 7, 2019

UKOSOAJI MKALI WA RAIS TAYYIP ERDOGAN WA UTURUKI KUFUATILIA VITISHO VYA MAREKANI VYA KUIONDOA NCHI HIYO KATIKA NATO

ErdoÄźan alitoa radiamali hiyo siku ya Ijumaa kufuatia matamshi ya hivi karibuni ya Mike Pence dhidi ya Uturuki ambayo imeazimia kununua ngao ya makombora ya S 400 ya Russia na kuongeza kwamba matamshi hayo ni kosa kubwa. Akizungumza mjini Washington kwa mnasaba wa kutimia mwaka wa 70 tangu kuundwa muungano huo, Pence aliitahadharisha Uturuki kutokana na sisitizo lake la kununua ngao hiyo ya makombora ya Russia kwa kusema: "Uturuki inatakiwa ichague ima kubakia ndani ya NATO au kununua ngao hiyo ya S400." Hii si mara ya kwanza kutolewa matamshi ya kuitaka serikali ya Ankara kuondoka katika Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi NATO. Ukweli ni kwamba tangu jeshi la Uturuki lilipoangusha ndege ya kivita ya Russia katika anga ya Syria, suala hilo la kuitimua Ankara katika muungano huo lilianza kushika kasi ambapo viongozi wa muungano huo wamekuwa wakijadili suala hilo kwa kipindi cha miaka minne sasa.
Hatua ya Uturuki kutaka kununua silaha za Russia, sababu ya kutimuliwa NATO
Baadhi ya weledi wa masuala ya kijeshi wa nchi za Magharibi wanasisitiza kwamba, muda wa kuiondoa Uturuki ndani ya muungano wa NATO sasa umewadia. Paul Valili, mtaalamu wa masuala ya kijeshi na jenerali mstaafu wa jeshi la Marekani ameieleza kanali ya televisheni ya Russia Today kwamba: "Siasa za Uturuki haziendi sawa na siasa za NATO na katika mazingira hayo chaguo la kuiondoa Ankara katika muungano huo ni linapewa kipaumbele hivi sasa." Pamoja na hayo bado kuna vizingiti viwili vikuu vya kuweza kuiondoka Uturuki katika muungano huo. Kizingiti cha kwanza ni kuwa, maamuzi yote ndani ya Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) huchukuliwa kwa namna ya mashauriano na baada ya kupigiwa kura ambapo Uturuki kama mwanachama inaweza kutumia kura ya Veto kukabiliana na aina yoyote ya maamuzi kma huo dhidi yake. Ama kizingiti cha pili ni hitajio kubwa la Umoja wa Ulaya kwa Uturuki. Hii ni kusema kuwa mwaka 2016 pande mbili zilitiliana saini hati ya makubaliano yanayohusiana na wahajiri haramu hati ambayo lengo lake ni kuwazuia wahajiri haramu kuingia barani Ulaya. Katika mazingira hayo tunaweza kusema kuwa, Uturuki ni mwanachama wa TANO ambaye kuna uwezekano mwingi akaendelea kusalia katika muungano huo wa kijeshi. Ni suala lisilo na shaka kwamba, vitisho vya Marekani kwa Uturuki vimeleta fursa nyingine kwa viongozi wa Ankara.
Trump na Mike Pence ambao wanataka kuitimua Uturuki kutoka NATO
Hii ni kusema kuwa kwa kuzingatia vitisho vya mara kwa mara vya viongozi wa Ankara hususan Rais Recep Tayyip ErdoÄźan vya kukabiliana na Marekani pamoja na Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO), sasa inaonekana kwamba viongozi wa Uturuki wamepata mazingira bora ya kuiwekea mashinikizo kambi ya Magharibi. Ukweli ni kwamba serikali ya Ankara imeingia katika mazingira ambayo inaweza kuyatunishia misuli madola ya Magharibi. Hii ni katika hali ambayo kwa mara kadhaa viongozi wa Uturuki wamekuwa wakijibu vitisho vya Wamagharibi kwamba watachukua hatua mbadala, ingawa katika vitendo vitisho, hivyo vya Ankara havijawahi kutoa changamoto yoyote kwa Magharibi hadi hivi sasa. Tunachokusudia kusema hapa ni kwamba, licha ya kuweko vitisho vya Marekani na Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) na pia marufuku ya kuiuzia Uturuki silaha, lakini bado serikali ya Ankara haijachukua hatua maalumu za kivitendo kuyalenga madola hayo ya Magharibi. Pamoja na hayo hivi sasa inaonekana kwamba, vitisho vya Marekani vya kuiondoa Uturuki katika muungano wa kijeshi wa NATO, vimeandaa mazingira ya kutekelezwa kivitendo na Uturuki, hatua mkabala wa hizo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages