LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 11, 2019

UCHAGUZI WA RAIS NCHINI ALGERIA KUFANYIK JULAI 4, 2019

Rais wa muda wa Algeria, Abdelkader Bensalah amesema, tarehe 4 Julai mwaka huu ndiyo siku ya kufanyika uchaguzi wa kumtafuta mrithi wa Abdelaziz Bouteflika, rais wa nchi hiyo aliyejiuzulu.
Tarehe ya kufanyika uchaguzi wa rais wa Algeria imetangazwa katika hali ambayo, siku ya Jumanne, bunge la nchi hiyo linalojumuisha Baraza la Seneti na Baraza la Taifa yalimchagua Spika wa Seneti Abdelkader Bensalah kuwa rais wa muda wa nchi hiyo.
Bensalah anashikilia wadhifa huo wa rais wa muda wa Algeria kwa muda wa siku 90.

Rais wa muda wa Algeria, Abdelkader Bensalah 

Kufuatia maandamano makubwa ya upinzani ya kupinga serikali yaliyofanyika kwa muda wa wiki sita nchini Algeria, hatimaye tarehe 2 Aprili Abdelaziz Bouteflika alitangaza rasmi uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wa urais baada ya kuweko madarakani kwa kipindi cha miaka 20.
Bouteflika mwenye umri wa miaka 82 na ambaye ni mgonjwa, mwezi Februari mwaka huu alitangaza kuwa atagombea tena urais kwa mara ya tano mfululizo. Kutangazwa uamuzi huo kuliamsha wimbi kubwa la maandamano ya upinzani nchini kote, ambayo awali yalikuwa ya kumshinikiza asigombee tena.
Hata hivyo licha ya kutangaza uamuzi huo, mkondo wa maandamano hayo ulibadilika na kuwa wa kumtaka ang'atuke rasmi madarakani.
Wakati huo huo, mara baada ya bunge la Algeria kumteua Spika wa Seneti kuwa rais wa muda wa kuandaa uchaguzi wa rais, maelfu ya watu waliandamana katika mji mkuu Algiers wakitaka timu nzima ya wanasiasa wenye ushawishi wa serikali ya Bouteflika waondoke madarakani na kufanyika mageuzi mapana katika mfumo mzima wa utawala wa nchi hiyo.../

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages