LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 15, 2019

SISITIZO LA KIONGOZI WA KOREA KASKZINI LA UDHARURA WA KUBADILISHWA SIASA ZA MAREKANI KUIHUSU PYONGYANG

Kiongozi huyo amesema kuwa, ili kuendelea mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini, Washington, inatakiwa kwanza ibadili siasa zake kuihusu nchi hiyo. Kim Jong-un ameongeza kwamba kushindwa mazungumzo na Marekani, kuna maana ya kuongezeka mizozo katika eneo la Rasi ya Korea. Amesema kuwa, hatopendelea kukutana na Rais Donald Trump wa Marekani, iwapo rais huyo hatofuata mwelekeo sahihi. Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini pia ameipa Marekani muda wa hadi mwishoni mwa mwaka huu (2019), iwe imechukua hatua madhubuti kwa ajili ya kubadilisha mazingira ya sasa sambamba na kufuata mwelekeo mpya kuihusu Pyongyang. Onyo la Kim Jong-un kwa Marekani juu ya udharura wa kubadilishwa siasa za nchi hiyo kuihusu Pyongyang, imetolewa baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kusisitiza kwenye kikao chake na Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini kwamba ataendelea kuiwekea vikwazo serikali ya Pyongyang.
Wakati Trump akitishia kuiwekea zaidi vikwazo Pyongyang, rais wa Korea Kusini naye anamshinikiza Trump aondoe vikwazo hivyo
Trump ametangaza msimamo huo, katika hali ambayo, Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini alikuwa amefanya safari nchini Marekani kwa ajili ya kumshawishi rais huyo wa Marekani kuiondolea Pyongyang baadhi ya vikwazo, suala ambalo hata hivyo halikufikiwa katika safari yake hiyo. Kuendelea misimamo ya uhasama ya Trump dhidi ya nchi hiyo ya Asia, kunajiri katika ambayo ilitazamiwa kuwa baada ya Washonton na Pyongyang kukubaliana kuendelea na mazungumzo yao, White House ingeiondolea baadhi ya vikwazo Korea Kaskazini kwa ajili ya kuleta hali ya kuaminiana na kwa ajili ya kuyafanya mazungumzo hayo yaweze kupiga hatua zaidi mbele. Siasa hizo za Rais Donald Trump za kupenda makubwa dhidi ya Korea Kaskazini ndizo zilipelekea kuvunjika duru ya pili ya mazungumzo kati ya Washington na Pyongyang nchini Singapore na Vietnam, licha ya kwamba Korea Kaskazini ilikuwa imeahidi kusimamisha majaribio yake ya silaha za nyuklia na makombora ya balestiki. Kwa kuzingatia siasa za vitisho na vikwazo dhidi ya nchi hiyo ya Asia, tangu kulipoanza mazungumzo ya nchi mbili hapo mwezi Juni mwaka jana nchini Singapore hadi sasa, na hasa kwa kuwa utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa ulifanywa na Pyongyang pakee, hivyo muhusika mkuu wa kuvunjika mazungumzo na kuendelea mgogoro wa Rasi ya Korea ni rais huyo wa Marekani.
Trump anaendeleza mabavu wakati Korea mbili zilikuwa zimeanza kuelewana
Kuhusiana na suala hilo, Andrey Ivanov mtaalamu wa masuala ya kisiasa nchini Russia na mwalimu wa mahusiano ya kimataifa amesema: "Kila kunapopatikana anga ya amani katika eneo la Rasi ya Korea, Marekani huwa inatoa tuhuma na matakwa mapya dhidi ya Korea Kaskazini. Ni kwa ajili hiyo ndio maana Korea Kusini na nchi nyingine zinazohusishwa na mzozo wa eneo hilo hususan China, zikawa zinasisitiza juu ya ulazima wa kubadilishwa siasa za uhasama za Washington hasa kwa kuzingatia kuwa ni nchi hiyo imekuwa ikijitapa kwamba imefungamana na misingi ya mazungumzo na Korea Kaskazini kwa ajili ya kuhitimishwa mzozo wa eneo hilo." Wasi wasi wa Korea Kusini ni kwamba, kufeli kikamilifu mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini kunakotokana na kupenda makubwa kwa White House na hakuna shaka kwamba, jambo hilo litauwa na matokeo hasi katika mwenendo wa utatuzi wa mgogoro kati ya Seoul na Pyongyang ulioanza tangu mwaka mmoja uliopita.
Kufanya mazungumzo na Trump ni kupoteza muda
Hasa kwa kuzingatia kuwa, Marekani imeweka wazi kwamba itayakubali makubaliano kati ya Korea mbili, iwapo serikali ya Pyongyang itafikia makubaliano na White House, suala ambalo ni vigumu kutekelezeka. Katika mazingira hayo ambapo Korea Kusini ina wasi wasi kutokana na ukwamishaji mambo wa Marekani kwenye njia ya mahusiano ya Korea mbili, kunaweza kuifanya Pyongyang kujiondoa kwenye mwenendo wa mazungumzo na ushirikiano mwema na jirani yake huyo. Suala hilo linapata nguvu pale ambapo Korea Kaskazini imetishia kujiondoa kwenye mazungumzo na ushirikiano na Korea Kusini, ili kwa njia hiyo iweze kuilazimisha serikali ya Seoul iishinikize Washington ili iachane na siasa zake za kupenda makubwa, vitisho na vikwazo sambamba na kujitenga mbali na White House kwa ajili ya kuhitimisha mzozo wa eneo la Korea.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages