LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 9, 2019

RAIS MAGUFULI ATAKA MAJESHI YATUMIKE KUHARAKISHA MAENDELEO

Rais John Pombe Magufuli amewataka Viongozi na Watendaji wa Wizara, Taasisi, Wakala na Mashirika ya Umma kuvitumia vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)katika  kazi za dharura zinazohitaji kasi ya haraka ya utekelezaji ili kuwaletea Maendeleo Watanzania.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kuchakata Mahindi katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mlale Mkoani Ruvuma leo Jumatatu (April 8, 2019), Rais Magufuli alisema JTWZ na JKT ni miongoni mwa majeshi ya vyombo vya ulinzi na usalama yanayofanya kazi zake kwa kasi kubwa katika miradi mbalimbali pindi wanapopewa dhamana na Serikali.

Aliongeza kuwa pamoja na majukumu yake ya msingi katika kusimamia masuala ya ulinzi na usalama, vyombo vya ulinzi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JTWZ) wakati wa hali ya usalama majeshi hayo yamekuwa yakitumika katika kutekeleza kazi za dharura pindi zinapotokea.

“Nawagiza Watendaji na Viongozi wa Wizara, Taasisi za Umma ndani ya Serikali kuvitumia vyema vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ikiwemo majeshi yetu ya JWTZ na JKT katika kutekeleza kazi za dharura zinatokea mara kwa mara, kwa mfano nimwemwagiza CDF sasa aunde magari ya zimamoto na kuyapeleka katika viwanja vyetu vya ndege ambapo ni miaka miwili sasa pamoja na zabuni yake kutangazwa na pesa kuwepo hakuna gari hiyo pale TAA (Mamlaka ya Viwanja vya Ndege)” alisema Rais Magufuli.

Akitolea mfano Rais Magufuli alisema kutokana na imani kubwa ya utendaji kazi wa JWTZ na JKT, Serikali imekuwa ikitoa zabuni za miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba na Ofisi za Serikali katika Miji ya Dar es Salaam, Dodoma na maeneo mengine ya nchi ambapo majeshi hayo yameweza kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi wa hali ya juu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages