Rais John Magufuli amewataka wafanyabiashara wadogo wenye vitambulisho vya ujasiriamali kutokubali kulipa tozo au ushuru wowote kwa watendaji wa Serikali.
Magufuli ameeleza hayo leo wakati akizungumza wananchi wa Migori mkoani Iringa kwenye ziara yake ya kikazi.
Kauli hiyo ya Rais Magufuli imekuja baada ya mwanamke mmoja kuelezea changamoto ya ushuru unaotozwa na manispaa katika biashara yake ya samaki licha ya kuwa na kitambulisho hicho.
Kufuatia malalamiko hayo, Rais Magufuli akatoa maelekezo kwa wajasiriamali wadogo wote kuwa wasikubali kutozwa fedha zozote kama wana vitambulisho hivyo vinavyowatambua rasmi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇