LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 13, 2019

POLISI: WATU 16 WAMEUAWA KWA RISASIKATIKA MAANDAMANO NCHINI SUDANI

Polisi nchini Sudan imesema kuwa, kwa akali watu 16 wameuawa huku wengine zaidi ya 20 wakijeruhiwa katika maandamano ya Alkhamisi na jana Ijumaa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
Hayo yamesemwa hii leo na Msemaji wa Polisi, Hashem Ali ambaye ameongeza kuwa, waandamanaji hao wameuawa kwa risasi na kwamba majengo ya serikali na ya kibinafsi pia yameshambulia na kuharibiwa katika maandamano hayo.
Mamia ya maelfu ya wananchi wa Sudan jana Ijumaa walimiminika katika barabara za Khartoum, katika maandamano ya kumtaka Jenerali Awad Mohamed Ahmad Ibn Auf, Waziri wa Ulinzi wa Sudan aliyetangazwa kuwa Kaimu Rais baada ya Omar al-Bashir kung'olewa madarakani ajiuzulu.
Tayari Jenerali Ibn Auf ametangaza kujiuzulu, huku akimteua Luteni Jenerali Abdel Fattah Burhan, Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Nchi Kavu kujaza nafasi yake.
Jenerali Awad Mohamed Ahmad Ibn Auf, Waziri wa Ulinzi wa Sudan
Baada ya kuapishwa juzi, Waziri huyo wa Ulinzi wa Sudan alitangaza kwamba, Baraza la Mpito la Kijeshi litaongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka miwili kabla ya kuitishwa uchaguzi mkuu, jambo ambalo liliamsha tena ghadhabu za wananchi waliomiminika mabarabarani kufanya maandamano, licha ya marukufu ya kutoka nje usiku.
Rais Omar Hassan al-Bashir aliyeingia madarakani mwaka 1989 kwa kumpindua kijeshi Sadiq al-Mahdi, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa wakati huo wa Sudan, alipinduliwa na jeshi la nchi hiyo na kuwekwa kizuizini, baada ya kushuhudiwa maandamano ya wananchi ya kumtaka ang'atuke uongozini baada ya miongo mitatu ya utawala wake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages