Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akifungua mkutano wa 94 wa klabu za rotary kanda ya 9211 uliokutanisha klabu wanachama kutoka Tanzania na Uganda katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa klabu za rotary zimekuwa zikifanya kazi kwenye sekta muhimu za maendeleo ya jamii hapa nchini ambayo yanaendana na vipaumbele vya Serikali katika Nyanja za kiuchumi, kijamii na maendeleo kwa ujumla.
“Natambua kuwa hapa nchini kuna klabu za rotary 38 zinazofanya kazi katika jamii kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma bora za maji, usafi na mazingira, kupambana na maradhi, kuokoa maisha ya mama na mtoto, elimu pamoja na kuwezesha vijana katika masuala ya kiuchimi” amesema Dkt. Ndugulile
Aidha Dkt ndugulile amezipongeza klabu hizo kwa kazi wanazofanya na kuzitaka klabu hizo kujikita zaidi kusiaidia Serikali katika mapambano dhidi ya magonjwa.
“Bado tuna ugonjwa wa malaria ambao umekuwa ukiathiri watu wengi hapa Tanzania na Duniani kwa ujumla, tunahitaji mchango wenu huko pia” alisema Dkt. Ndugulile. Kwa upande wake Mwakilishi wa wa Rais wa Klabu ya Rotary Duniani Bi. Dean Rohrs amesema kuwa klabu hizo zipo kwa ajili ya kuhudumua jamii kwa kuhakikisha wanatafuta vyanzo vya fedha kuweza kusaidia katika upatikanaji wa huduma muhimu ndani ya jamii.
Naye Gavana wa Kanda ya 9211 Bi. Sharmilla Bhatt amesema kuwa kanda yake imekuwa ikitoa misaada mbali mbali kwa jamii na kuihaidi Serikali kuwa itendelea kutoa ushirikiano katika kusaidia upatikanaji wa huduma muhimu huku akisema kuwa milango iko wazi kwa wenye nia ya kutaka kujiunga na klabu za rotary ili kuboresha maisha ya jamii.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇