Waziri wa TAMISEMI Seleman Jafo ametoa maagizo ya siku 30 kuhakikisha halmashauri zote 67 zilizo na ujenzi wa hospitali za wilaya ziwe zimeshafikia hatua ya lenta kwa majengo yote Saba kwa kila Halmashauri na yawe yamefikia
hatua ya upauaji..
Waziri Jafo ametoa Maagizo hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amebainisha kuwa kuna uzembe mkubwa wa ujenzi wa hospitali hizo za Wilaya licha ya serikali kutoa Tsh.Bil.1.5 kila wilaya ambapo ni sawa na Tsh.Bilioni 105 kwa wilaya 67 .
Hivyo Waziri Jafo amesema kufikia Tarehe 12 Mei lazima kila halmashauri itemize maagizo hayo .
Aidha ,Waziri Jafo ameagiza mikoa yote kufikia Tarehe 14 Mei ,2019 iwe imeshatuma picha za Majengo yote ofisi ya TAMISEMI Makao Makuu na Tarehe 27 Mei,2019 mikoa yote iwe imeshatuma Picha ya Majengo yote yaliyokamilika katika wilaya husika na Tarehe 13 Mei hadi Tarehe 25 Mei Majengo yote yawe yameshapauliwa na Tarehe 27 Mei ,mikoa yote iwe imeshatuma picha zote za Majengo yote yaliyokamilika na Tarehe 28 Mei Wizara iwe imeshapata Picha za Majengo Yote ya Hospitali.
Ikumbukwe kuwa,Halmashauri zote 67 zenye ujenzi wa hospitali za wilaya zinatakiwa ziwe zimeshakamilisha ujenzi ifikapo Juni 30 ,Mwaka huu na majengo yawe tayari kwa Matumizi, ambapo kila halmashauri imepewa Tsh.Bil.1.5 Kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇