LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 24, 2019

CCM IRINGA YAMTAKA MBUNGE PETER MSIGWA KUFANYA MUTANO WA KUWAAGA WANANCHI

 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CCM Mkoa wa Iringa

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza amesema amemtaka mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa, kufanya mkutano wa hadhara ili kuwaaga wananchi kwa kuwa zama za kuiongoza manispaa ya Iringa umefika kikomo.

“Zama za Msigwa zimeisha kuongoza manispaa ya Iringa kwa kuwa wananchi wameshamchoka kwa kuwa sio kiongozi aliyewasaidia kuleta maendeleo kwani toka aingie madarakani hajawahi kufanya maendeleo yeyeto yale kwenye jimbo hili la Iringa” alisema Baraza

Baraza alisema kuwa chama cha mapinduzi kinasema hivyo kwa kuwa chama cha mapinduzi kipo imara kweli kutokana na aina ya uongozi walionao na mfumo wa siasa ambao wamekuwa wakiutumia kuwafikia wananchi wa mkoa wa Iringa.

“Saizi tumefanikiwa kuwafikia wananchi wa chini kabisa ambao kunakipindi huwa wanasaulika wakati ndio wapiga kura wetu hivyo tumerudi tumejipanga na tunaendelea kufikia kila siku kwa kupokea changamoto zao” alisema Baraza

Lakini pia Baraza alisema kuwa wapinzani wamekuwa hawana jambo jipya ambalo wanaweza kuliteleza kwa kuwa serikali ya chama cha mapinduzi kimesimamia vilivyo serikali na kuhakikisha wanatatua changamoto za wananchi waliowapa mamlaka ya kuwaongoza.

“Wapinzani saizi kazi yao ni kueneza propaganda chafu ambazo sasa wananchi wamezichoka na hazina nafasi kwenye ulingo wa siasa safi na yakuleta maendeleo kwa wananchi” alisema Baraza

Baraza alisema kuwa chama cha mapinduzi sio dhaifu kwa kuwa kimefanikiwa kupata madiwani saba ambao wameamia kwenye chama cha mapinduzi kwa ajili ya udhaifu wa CHADEMA  na viongozi wake wa mkoa wa Iringa.

“Moto wetu ndio kwanza umeanza hivyo tumwambie Msigwa ajipange kuondoka kwa kuwa saizi ameshakuwa dhaifu na hana jambo jipya ambalo linaweza kusaidia kuleta maendeleo kwa wananchi wa mkoa wa Iringa” alisema Baraza

Hoja hiyo imekuja siku kadhaa  baada mbunge wa jimbo la Iringa kusema kuwa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa ni dhaifu na hakiwezi kumuondoa madarakani labda yeye aamue kung’atuka kwa hiyari yake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages