Matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi moja ya nchini Marekani inayojulikana kwa jina la Rand Corporation yanaonyesha kuwa Marekani itashindwa vibaya na kupata kipigo kikali iwapo kutajiri vita katika siku za usoni.
Taasisi ya Rand Corporation imezungumzia pia ukiukaji mbalimbali wa sheria unaofanywa Marekani na kushindwa nchi hiyo kukabiliana kiusalama na nchi nyingine kama Russia na China. Muhtasari wa utafiti wa taasisi hiyo yenye mkataba na Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon unaonyesha kuwa: Marekani itashindwa vibaya iwapo vita vya Tatu vya Dunia vitatokea na haitakuwa na uwezo wa kukabiliana na Russia na China.
Taasisi ya Rand Corporation imechunguza pia senario mbalimbali kuhusu uwezo wa Marekani wa kupambana vitani na kufikia natija kwamba, ingawa gharama za kijeshi za nchi hiyo zimepindukia dola bilioni 700 kwa mwaka lakini wazi kuwa Marekani itapata maafa makubwa iwapo kutatokea vita.
Muswada wa bajeti ya mwaka huu ya Marekani uliowasilishwa mbele ya baraza la kongresi la nchi hiyo umepelekea kuongezwa gharama za matumizi ya kijeshi kwa kupunguzwa bajeti ya matumizi ya masuala mengineyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇