LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 5, 2019

STAKABADHI ZA RAIS TRUMP ZACHUNGUZWA



Kamati ya sheria ya bunge la Marekani inamchunguza Rais Donald Trump kuhusiana na uwezekano wa matumizi mabaya ya afisi.

 Mkuu wa kamati hiyo wa chama cha Democratic Jerry Nadler amesema kufikia sasa mashirika 81 na watu binafsi wameitishwa stakabadhi kuhusiana na suala hilo.

Miongoni mwao ni watoto wa kiume wa Trump Donald Junior na Eric, ambao tangu achukue mamlaka wamekuwa wakiongoza kampuni ya Trump Group, pamoja na mkwe wake Jared Kushner.

Nadler amesema Rais Trump anakwenda kinyume na kanuni za maadili karibu kila siku ingawa hajaitwa na bunge kuelezea kuhusiana na mambo hayo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages