WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Profesa Palamagamba John Kabudi amesema mabadiliko ya sheria yaliyofanyika
hivi karibuni katika sekta za madini, maliasili na uwekezaji yana lengo la
kuweka mazingira bora yatakayoleta tija kwa Taifa na wawekezaji kuondoa utaifishaji (nationalization) na upokonyaji mali
(confiscation).
Kabudi (kulia), meyasema hayo wakati wa
mazungumzo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited Lynda
Chalker (kushoto) na kuongeza kuwa hatua zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya Tano
chini ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli ni kuweka uwanda sawa kwa
kuondoa rushwa na urasimu na kumtaka Mhe Chalker kuhamasisha wawekezaji kutoka
Uingereza kuja kuwekeza hapa nchini.
Katika mazungumzo hayo Profesa Kabudi
amemuahakikishia Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya Africa Matters limited
kuwa mazingira ya uwekezaji nchini ni salama na yameboreshwa zaidi na hakuna
masuala ya utaifishaji (nationalisation) wala upokonyaji mali (confiscation)
kama inavyopotoshwa na baadhi ya watu wasioitakia mema Tanzania.
“Katika
kutekeleza diplomasia ya Uchumi Tanzania inatoa kipaumbele kwa uwekezaji wenye
tija kwa Taifa na unaozingatia maslahi ya pande zote (Win – win situation) kwa
kuwa sasa kupitia sheria mpya tuna mfumo wa kodi unaofahamika, misamaha ya kodi
isiyo na upendeleo na si kweli kuwa mazingira yamebadilika na kusema kweli
kilichbadilika ni usimamizi madhubuti,kupambana na rushwa na kuhakikisha kodi
stahiki inalipwa” Amesema Kabudi
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited Lynda Chalker amempongeza Rais Dkt Magufuli kwa kuboresha
mazingira ya uwekezaji nchini na kuongeza kuwa atakaporejea Uingereza msafara
wa wafanyabiashara na wawekezaji kuja Tanzania na kwamba kuna uwezekano mkubwa
wa uwepo wa mabadiliko ya kisiasa nchini Uingereza na marafiki wa Jumuia ya
madola kama Tanzania wanapewa kipaumbele katika uwekezaji na ujenzi wa viwanda.
“Ninadhani
wawekezaji hasa wa nje ya Tanzania wanahitaji kufanya utafiti kidogo kuhusu
kile Tanzania inachokihitaji na namna watakavyonufaika kwa kuwekeza
Tanzania,nimuahidi waziri hapa kuwa nitakaporejea London, nitakutana na mjumbe
maalum wa Uingereza wa mambo ya biashara kwa Tanzania pia nitaonana na mawaziri
wa mambo ya nje wa Uingereza na Jumuia ya Madola kuona uwezekano wa kuwa
na mkutano mkubwa ambao utazungumzia zaidi masuala ya uwekezaji na biashara kwa
Tanzania”
TIC ifike huku vijijini tupo wakulima wadogo wenye ekari kati ya hamsini na mia ambao tungependa kushirikiana na wawekezaji wa kati katika ufugaji na ukulima wa organic wa mboga,kuku,etc
ReplyDelete