LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 10, 2019

SHAHIDI WA KIPÀLESTINA AUAWA KWA RISASI NA WANAJESHI WA ISRAEL

Kijana wa Kipalestina ameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Wizara ya Afya ya Palestina imesema kuwa, kijana huyo wa miaka 22 aliyeuawa shahidi alikuwa anafahamika kama Salameh Salah Kaabneh.
Shirika la habari la Palestina la Wafa limetangaza kuwa, mauaji hayo ya kikatili yamefanyika mapema leo kaskazini mwa mji wa Ariha (Jericho).
Polisi ya utawala haramu wa Israel inadai kuwa, kijana huyo wa Kipalestina aliyekuwa amefunika uso wake ameuawa baada ya kukataa kusimama katika kituo cha upekuzi.

Wanajeshi wa Israel wakimkandamiza kijana wa Kipalestina

Haya yanajiri chini ya wiki moja baada ya vijana wengine wawili wa Kipalestina kuuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala huo katili katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamekuwa yakikosoa mienendo ya kikatili ya maafisa usalama wa utawala bandia wa Israel, haswa namna wanavyoamiliana na Wapalestina.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages