Serikali ya Tanzania kupitia Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imefanikiwa kuimarisha usimamizi na udhibiti wa matumizi ya Teknolojia ya Nyuklia nchini.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekenolojia Mheshimiwa William Ole Nasha ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa waratibu wa miradi ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia kutoka nchi 46 wanachama wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki ( IAEA ) unaofanyika jijini Arusha.
Naibu waziri Ole Nasha amesema Shirika hilo linafadhili miradi mingi katika sekta mbali mbali hapa nchini ikiwemo sekta ya afya ambapo imewezesha kupatikana kwa vifaa mbali mbali vya uchunguzi wa tiba na maradhi ya saratani ambavyo vimefungwa katika hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando Jijini Mwanza na Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na vifaa vya uchunguzi katika hospitali hizo mbili, pia taasisi nyingine mbalimbali zimepata vifaa vya maabara ambapo kwa ujumla wake vifaa vyote vina thamani ya kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 6.2 na pia kutoa mafunzo kwa wataalamu katika eneo la matumizi ya mionzi na Teknolojia ya Nyuklia mpango ambao uligharimu Shilingi za Tanzania Bilioni 3.3.
Pia amelishukuru na kulipongeza shirika hilo kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya mataifa wanachama hususan kwa utaratibu wake wa kuwa na mikutano inayowezesha kubadilishana uzoefu baina ya wanachama. amewataka washiriki wa mkutano huo kuhakikisha wanafanya majadiliano yenye tija kwa lengo la kusaidia nchi zao kwenye udhibiti na matumizi salama ya teknolojia ya nyukulia
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA ) Profesa Shaukat Abdulrazak amesema wataendeela kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha matumizi salama ya teknolojia ya Nyukilia kwenye sekta mbali mbali ikiwemo sekta ya Afya , Kilimo,Mifugo,Maji ,Viwanda na Ujenzi, Mkutano huo wa Siku tano utamalizika tarehe 15 , Machi 2019.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇