LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 30, 2019

RAIS MAGUFULI NA AMIRIJESHI MKUU ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA 146 WA JWTZ IKULU DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Dkt John Magufuli, leo Machi 30, 2019, amewatunuku Kamisheni Maofisa Wanafunzi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).


Rais Magufuli amewatunuku Kamisheni katika cheo cha Luteni USU maafisa hao wanafunzi ambao idadi yao ilikua 146.

Hafla ya utunukiwaji kamisheni kwa Maafisa hao imefanyika katika viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Brigedia Jenerali Steven Mnkande wakati wakielekea kwenda kupiga picha za kumbukumbu Ikulu jijini Dar es Salaam.


 Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakila kiapo cha Utii mbele ya Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutunukiwa Kamisheni Ikulu jijini Dar es Salaam.
Maafisa Wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Wakivalishana vyeo mara baada ya kutunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika tukio lililofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amiri Jeshi Mkuu  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli Brigedia Jenerali Steven Mnkande wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Maafisa wapya wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania mara baada ya kutunukiwa Kamisheni Ikulu jijini Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU).


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages