Jeshi la Magereza nchini
limekanusha vikali taarifa iliyodai kwamba wafungwa wa kiume
wanaingiliana kimwili katika Gereza Shinyanga na kusema kuwa taarifa hiyo siyo
ya kweli.
Taarifa maalum toka ofisi ya
kamishna Jenerali wa Magereza inasema kuwa habari hiyo ya upotoshwaji
imechapishwa na gazeti la nipashe lenye namba ISSN 0856 NA. 0579874 la
tarehe 25 Machi, 2019 katika ukurasa wake wa kwanza ikisomeka kwamba “MAGEREZA YAKIRI TATIZO WAFUNGWA KUINGILIANA”.
Pia, katika
ukurasa wa pili (02) wa gazeti hilo, imeelezwa kuwa wafungwa wa kiume
katika Gereza la Mkoa wa Shinyanga (Mhumbu), wamedaiwa kufanya ngono
kinyume na maumbile, hali iliyoelezwa kuchangia maambukizi ya magonjwa ikiwemo
virusi vya UKIMWI.
"Ieleweke
kuwa aliyenukuliwa kutoa taarifa hiyo, Ofisa wa Dawati la Jinsia la
Magereza Mkoa wa Shinyanga, Victoria Kizito siyo Msemaji wa Jeshi la Magereza na
hana mamlaka ya kutoa wala kudhibitisha habari wala taarifa kwa niaba ya Jeshi." Imesisitiza taarifa hiyo.
Imeeleza Sheria za nchi ikiwemo Sheria na kanuni za Jeshi la Magereza zinakataza vitendo
vya aina hiyo kwa vile ni kosa la jinai.
"Vitendo hivyo
vinadhibitiwa ndani ya magereza kwa kuwaelimisha wafungwa madhara yake na pindi
kunapotokea jaribio la mfungwa kujihusisha na vitendo hivyo, Mhusika
huchukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za Jeshi ikiwa
ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria."
Mwisho Jeshi hilo limevikumbusha Vyombo vya habari na waandishi kuwa taarifa zinazolihusu
Jeshi la Magereza hutolewa au kuthibitishwa na Kamishna Jenerali wa
Magereza au Msemaji wa Jeshi,
hivyo taarifa zozote zinazotolewa nje ya utaratibu huo
zisipokelewe.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇