Maalim Seif Sharif Hamad
Utata na hatma ya mali hizo unafuatia Katibu Mkuu huyo kuzikana mali za CUF zikiwemo ofisi za makao makuu ya chama hicho zilizopo Zanzibar akidai kuwa ofisi hizo zilikodiwa na hazikuwa mali ya chama.
Maalim amesema hatma ya umiliki wa majengo hayo ipo mikononi mwa mmiliki wa majengo hayo.
Maalim ametangaza kujiunga na ACT-Wazalendo leo Jumatatu, Machi 17, 2019 kwenye mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi za wabunge wa CUF zilizopo Magomeni, jijini Dar es Salaam.
Uamuzi huo wa gwiji hilo la siasa nchini Tanzania umekuja saa chache tu baada ya Mahakama Kuu nchini Tanzania kumthibitisha Haruna Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho.
Uamuzi huo wa mahakama kuu wa kumtambua Lipumba ulileta taharuki kwa wafuasi wa CUF wanaomuunga mkono Maalim ambao walikuwa hawamtaki Lipumba.
Maalim amesema yeye na viongozi wenzake wamefikia maamuzi hayo ya kujiunga na ACT baada ya kuvitembelea vyama kadhaa vya siasa kabla hawajafanya maamuzi ya kujiunga na ACT – Wazalendo.
Kiongozi huyo aliyekuwa mgombea wa CUF nafasi ya Urais Zanzibar tangu mwaka 1995, amewataka wanachama wote wa CUF wanaomuunga mkono kujiunga na ACT – Wazalendo.
“Nyumba uliyoizoea ni ngumu kuihama. Ila inafika mahala lazima ufanye maamuzi. Tumeamua kuiacha nyumba yetu ya zamani na sasa tupo kwenye nyumba mpya.
“Tulichofanya ni kushusha nanga na kuong’oa nanga. Dhamira yetu ya mapambano ipo pale pale ila sasa tunayafanya kwenye chombo kingine,” amesema Maalim Seif.
Kwa habari zaidi soma link ifuatayo;
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇