Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo amefanya ziara ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya katika Hospitali Temeke na Hospitali ya Manispaa ya Mbagala Jijini Dar es salaam.
Kwa kiasi kikubwa Dkt. Ndugulile ameonekana kuridhishwa na hali ya utoaji huduma hususani katika hali ya upatikanaji wa dawa, huku akisisitiza kuwa dawa zote muhimu zipo za kutosha na zinapatikana katika Hospitali zote na vituo vya afya vya Serikali bila malipo.
Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali imeongeza bajeti ya dawa, vifaa na vifaa tiba kutoka Billion 30 mpaka bilioni 270 tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani ili kurahisisha matibabu kwa Wananchi.
Aidha, Dkt. Ndugulile amemwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke Dkt. Gwamaka Mwabulambo kuhakikisha anasimamia vizuri utoaji huduma katika Hospitali hizo ikiwemo kila asubuhi kuhakikisha wanaandika dawa zote zilizopo.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇