Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam.
Rais Dk. John Magufuli, amemteua Balozi Dk. Augustine Mahiga (kulia)kuwa Waziri wa Sheria na Katiba huku Profesa Palamagamba Kabudi aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo akiteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kabla ya Rais Dk. Magufuli kufanya mabadiliko hayo madogo ya Baraza la Mawaziri, Dk. Mahiga ndiye aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kwa tafsiri nyingine ni kwamba mawaziri hao wamebadilishana nafasi.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo tarehe 03 Machi, 2019 imesema, Mawaziri Wateule hao wataapishwa kesho tarehe 04 Machi, 2019 saa 3:30 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Your Ad Spot
Mar 3, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇