
Huduma za Elimu ya afya ya kinywa na meno, uchunguzi na ushauri zitatolewa bila malipo kwa Wananchi katika mikoa mbalimbali nchini.
Kitaifa Maadhimisho yatafanyika Mkoani Arusha ambapo pia matibabu ya kinywa na meno yatatolewa bila malipo kwa Wananchi.
Tarehe 17 Machi 2019 matembezi ya uhamasishaji wa afya ya kinywa na meno yataanza Saa kumi na mbili Asubuhi kutoka viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha mpaka Viwanja vya Shule ya Msingi Meru na yataongozwa na Mhe. Mrisho Gambo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kilele cha Maadhimisho tarehe 20 Machi 2019 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Meru, Mgeni Rasmi atakuwa Mh. Selemani Jafo (Mb), Waziri katika Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Wote mnakaribishwa
Sema Ahh: Chukua hatua zinazozingatia Afya ya Kinywa na Meno"
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇