LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 13, 2019

WAZIRI DKT. KALEMANI ATOA “DEADLINE” KIGAMBONI NAO WAPATE UMEME WA UHAKIKA.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umneme cha Kurasini jijini Dar es Salaam, itakuwa ndio suluhisho la tatizo la upatikanaji umeme kwa watu wa Kiamboni.
Dkt. Kalemani ameyasema hayo leo Februari 13, 2019 wakati alipofanya ziara ya kukagua kituo hicho ili kujua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mradi huo.
“Niwape uhakika wananchi wa Kigamboni, kukamilika kwa mradi huu kutaleta suluhishi kubwa sana kwa wananchi wa Kigamboni, huu mradi unaweza kuhudumia wananchi elfu  tisa (9000) kwa wakati mmoja na tayari tunahudumia wananchi elfu tano 5000 kwa hiyo tutakuwa na takriban wananchi elfu kumi na nne 14000 kwa Kigamboni watakaokuwa wanahudumiwa na umeme kutoka hapa.” Alisema.
Hata hivyo Dkt. Kalemani alimuonya mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha kazi hiyo inakamilika haraka iwezekanavyo ili kuwaondolea adha ya upatikanaji wa umeme wananchi wa Kigamboni.
Tunataka mradi huu ukamilike, tarehe 10 mwezi Machi mwaka huu saa saba mchana nitakuja kuwawashia umeme wananchi wa Kigamboni na Mheshumiwa Mbunge Ndungulile nitamualika.” Aliagiza.
Hili ni agizo la mwisho na sitarudi hapa kukagua na kwabahati nzuri kero ya umeme kwa Dar es Salaam eneo lililobaki ni Kigamboni, alisema Dkt. Kalemani.
Kulikuwa na sub station takriban tano na zote zimekamilika isipokuwa huu, kwa hiyo kuanzia kesho weka vibarua na mfanye kazi usiku na mchana ili kukamiulisha kazi iliyobaki.” Alisema.
Akizungumzia hali ya utekelezaji wa mradi huo na jinsi watakavyotekeleza maagizo ya Waziri, Meneja Miradi wa TANESCO anayeshughulikia uzalishaji, Mhandisi Stephene S.A. Manda alisema, watahakikisha wanatekeleza agizo la Mheshimiwa waziri na watahakikisha kabla ya tarehe 10 kazi hiyo itakamilika kwani vikwazo vilivyosababisha kuchelewa kwa mradi vimetatuliwa.
“Kwakweli kama alivyosema Mheshimiwa waziri, huu mradi ulianza siku nyingi sana na kilichotuchelewesha ni kufidia eneo moja ambalo muhusika alitaka alipwe asilimia 47 ya bajeti yote ya compensation (fidia) kwa hiyo alituchelewwesha karibu mwaka mzima lakini waziri alipokuja Novemba mwaka jana (2018) alitoa agizo tukutane na muhusika ili tuongee na tulifanya hivyo na tukakubaliana na kumlipa na ndio maana unaona nguzo ziko tayari kilichobaki ni kuvuta waya na kuvusha bahari na nikazi ambayo haitachukua muda mrefu.” Alisema Mhandisi Manda.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), akiongozwa naMeneja Miradi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, anayeshughulikia uzalishaji (Generation) Mhandisi Stephene S. A. Manda (aliyenyoosha mikono), wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa minara ya kupitisha umeme kutoka kwenye kituo cha kupoza na kusafirisha umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam leo Februari 13, 2019.
 Waziri Dkt. Kalemani (kushoto) na   Naibu Mkurugenzi Mtendaji (anayeshughulikia usafirishaji), Mhandisi Issack Chaji (katikati)wakimsikilzia Mhandisi Manda kuhusu kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho na kueleza kuwa imebaki kazi ya umaliziaji.
 Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Mhandisi Manda, akk patia maelezo Dkt. Kalemani kuhusu njia ya kupeleka umeme eneo la Kigamboni kutoka kituo hicho cha Kurasini.
 Waziri Dkt. Kalemani akizungumza mara baada ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi w akituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, (anayeshughulikia usafirishaji), Mhandisi Issack Chaji, (kushoto), akizungumza jambo na Meneja Miradi wa Shirika hilo, Mhandisi Stephene S.A. Manda

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages