LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 24, 2019

WATU 150 WAFARIKI INDIA

Watu wengine 150 wamefariki dunia baada ya kunywa pombe iliyo na sumu kaskazini mashariki mwa India, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na hospitali tatu kwenye jimbo la Assam, ambako watu wengine wanaendelea kupatiwa matibabu. Tukio hilo ni la pili kuripotiwa mwezi huu. Mamlaka zilikadiria kwamba watu 84 walifariki jana Jumamosi. Waziri wa afya wa jimbo hilo amesema watu wengine 170 wamelazwa hospitali na wengine wakizidi kupokelewa kutoka maeneo ya karibu. Janga hilo linakuja katika kipindi cha wiki mbili baada ya watu wengine 100 kufariki kwa sababu ya kunywa pombe yenye sumu kwenye majimbo mawili ya Kaskazini mwa India . Vifo vinavyotokana na unywaji wa pombe za kienyeji nchini India hutokea mara kwa mara ambako watu wengi hawawezi kumudu pombe zenye majina.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages