NA KHAMISI MUSSA
Vyuo Vikuu vya Afya na Sayansi Shirikishi hapa nchini vinatarajiwa kuanza kutumia mtaala mmoja kufutia kupatikana kwa mradi mpya wakuwafikia walengwa katika mageuzi ya Utoaji Elimu ya fani za Afya.
Hayo yamesemwa leo na Mtafiti mkuu wa mradi huo Profesa Ephata Kaaya katika Uzinduzi wa mradi huo ambao umefadhiliwa na Shirika la Afya la Marekani.
Katika uzinduzi huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) Jijini Dar es Salaam Profesa Kaaya ambaye ni Makamu Mstaafu Chuo hicho alisema mradi huo unalenga kuwafikia walengwa katika Mageuzi ya Utoaji Elimu ya fani za Afya hapa nchini.
Alisema mradi huo utaanza kuboresha zaidi elimu ya afya katika vyuo vya MUHAS, KCMC Bugando na baadaye katika vyuo vyote nchini hali itakayo wezesha kutotohautiana kwa mitaala katika vyuo vyote nchini
"Kilichofanyika hapa ni kufungua kuanza kwa wakati wa mradi huu uliofadhiliwa na Shirika la Afya la Marekani ambapo kazi yake kubwa ya huu mradi ni kuboresha Ufundishaji wa Elimu za afya na kuboresha mtaala kwa ufanisi zidi na uboreshaji wa walimu" alisema Profesa Kaaya.
Alisema hatua hiyo baadaye itawezesha kupatikana wataalam wa afya wenye kuweza fanya kazi kwa umahiri kuliko ilivyo sasa na kufafanua kuwa wakati wa kufanya kazi
katika mradi huo watakuwa wakishirikishwa wadau wote na ikiwemo mabaraza ya taaluma za afya kama TCU na wadau wengine wote wakiwemo walimu na wanafunzi.
Mtafiti Mkuu wa Mradi wa kufikia walengwa katika Mageuzi ya Utoaji Elimu ya fani za Afya Tanzania, Profesa Ephata Kaaya akizungumza na wadau wakati wa uzinduzi wa mradi huo, katika ukumbi wa MUHAS Dar es Salaam, leo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
PICHA ZAIDI>BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇