LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 2, 2019

VIONGOZI WA UVCCM WILAYA YA KINONDONI WATEMBELEA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE (JKCI)

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi Robert Mallya wakizungumza na Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni walioongozana na Msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018, Maria Manyama walipotembelea taasisi hiyo Februali 1, 2019 Jijini Dar es Salaam.
 Daktari bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Vivian Mlawi akielezea namna chumba cha ICU kinavyowahudumia wagonjwa waliotoka katika chumba cha upasuaji kwa viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kinondoni walioongozana na Msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018 Maria Manyama walipotembelea taasisi hiyo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Shirikishi na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Delila Kimambo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akiongea jambo na  Msichana wa kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne 2018 Maria Manyama mwenye ndoto ya kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alipotembelea taasisi hiyo pamoja na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kinondoni  Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wa taasisi hiyo wakiwa  katika picha ya pamoja na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Kinondoni baada ya kufanya ziara katika taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo ziara. (PICHA NA JKCI)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages