Tume ya uchaguzi nchini Nigeria imeharisha zoezi la upigaji kura kwa kile walichoeleza kuwa wanafanya hivyo ili kuweka mipango sawa.
Hatua hiyo inakuja zikiwa ni Saa tano kabla ya kuanza zoezi la upigaji kura.
Nchi hiyo yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, uchaguzi wake uliokuwa ufanyike leo Feburay 16, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Mahmood Yakubu ndiye ametangaza uamuzi huo.
Kuna wagombea 72 wa kiti cha urais, lakini mshindani mkuu ni Atiku Aboubakar, ikiwa ni mara yake ya nne kugombea kiti hiko, na Rais wa nchi hiyo kwa sasa, Mohamud Buhari ambaye ameahidi kupeleka nchi hii katika hatua nyingine endapo atachaguliwa tena kwa kipindi cha miaka minne.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇