Kanisa Katoliki halitafumbia macho vitendo vya kulawiti watoto vinavyofanywa na mapadri kama ilivyozoeleka siku za nyuma, amesema kiongozi wa kanisa hilo ulimwenguni Papa Francis katika hotuba ya kuhitimisha mkutano wa kilele wa kupambana na unyanyasaji kingono dhidi ya watoto mjini Vatican. Hata hivyo hotuba yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu haikutoa mwangaza wa hatua thabiti juu ya tatizo hilo. Mkutano huo uliitishwa kutokana na wimbi la madai ya unyanyasaji kingono na kufichwa kwa madhambi hayo, nchini Marekani, Chile, Ujerumani na Australia. Papa Francis amesema hakuna unyanyasaji ambao utafichwa kama ilivyozoeleka kipindi cha nyuma au kufumbiwa macho kwasababu vitendo hivyo ni ushetani na vinazidi kulichafua kanisa hilo. Mwanzoni mwa mkutano huo Papa aliwasilisha mpango wenye vifungu 21 wa kushughulikia kashfa hiyo, lakini hata hivyo hotuba yake ya leo haikutaja hatua mahususi mbali ya kusema Vatican itaimarisha sheria zake kupambana na picha za kingono za watoto mtandaoni.
Your Ad Spot
Feb 24, 2019
PAPA FRANCIS: KANISA KATOLIKI HALITOFUMBIA MACHO VITENDO VYA ULAWITI
Tags
Kimataifa#
Share This
About Khamisi Mussa
Kimataifa
Tags
Kimataifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇