LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 9, 2019

NAIBU WAZIRI MASAUNI AFUNGUA SEMINA YA VIONGOZI WA TAASISI ZA KIISLAM JIJINI DAR ES SALAAM

Na Mwandishi Wetu
Serikali imesema haitakua tayari kuona Amani na Utulivu wa Nchi inachezewa  huku ikisisitiza uwepo wa Umoja kati ya wananchi bila kujali tofauti ya imani, kabila au itikadi yoyote.
Hayo yamesemwa  na  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akifungua Semina ya siku mbili iliyofanyika jijini Dar es Salaam ikiwahusisha  Viongozi wa Taasisi za Kiislamu lengo ikiwa ni kuwakumbusha kuhubiri amani katika sehemu zao
Amesema muelekeo na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kukuza maendeleo katika sehemu mbalimbali nchini lengo ikiwa kuinua maisha ya wananchi nan chi kwa ujumla
“Serikali hii imejidhatiti kuhakikisha maendeleo yanakuja kwa kasi na maendeleo hayawezi kuja ikiwa amani na utulivu haupo, sisi kama serikali tutahakikisha tunalinda amani iliyopo ili wananchi wapate kufanya shughuli za kiuchumi bila wasiwasi wowote” alisema Masauni
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum aliihakikishia serikali kutokuwepo kwa mifarakano kati ya taasisi mbalimbali kama ilivyokuwepo awali huku akisisitiza kuendelea kwa umoja huo ili jamii ipate kuendelea
“Sisi kama Bakwata tunaihakikishia serikali uwepo wa umoja na ushirikiano baina ya baraza na taasisi zingine na tofauti zetu hazipelekei kukoseana au kuvunjiana heshima kwahiyo tunaomba serikali iamini uwepo wa maelewano mazuri tu kwa maendeleo ya nchi hii” alisema Sheikh Mussa
Semina hiyo ya Siku mbili imejumuisha viongozi wa Taasisi mia moja huku mada ya Nafasi ya Taasisi za Kiislam katika Kuleta Umoja na Kuishi kwa Amani itajadiliwa.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) akisalimiana na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum baada ya kuwasili katika Ufunguzi wa Semina ya Viongozi wa Taasisi za Kiislam, uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Viongozi wa Taasisi za Kiislam, ambapo aliwahakikishia uwepo wa Amani na Utulivu nchini.Ufunguzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Mussa Salum akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Viongozi wa Taasisi za Kiislam, ambapo  aliihahakikishia serikali kuwepo kwa maelwano kati ya taasisi mbalimbali za dini lengo ikiwa ni kurahisisha maendeleo nchini.Ufunguzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Viongozi wa Taasisi za Kiislam, ambapo  aliwahakikishia uwepo wa Amani na Utulivu nchini.Ufunguzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages