LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 25, 2019

MKOA WA MARA WAJIPANGA KUKOMESHA VITENDO VYA UKATILI

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Vicky Mbunde (wa pili kulia) akifungua kikao cha Kamati ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto ya Mkoa wa Mara kilichofanyika leo Mjini Musoma. wakwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Sebastian Kitiku 
Katibu Tawala msaidizi Utawala na Rasilimali Watu mkoa wa Mara Bi. Clothilde Komba (kushoto) akizungumzia umuhimu wa kikao cha Kamati ya Mkoa ya ulinzi wa Wanawake na  Watoto kilichofanyika leo Mjini Musoma.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Sebastian Kitiku (kulia) akizungumza jambo na wadau juu ya umuhimu wa ujumbe katika kuleta hamasa kwa jamii katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kikao kilichofanyika leo mjini Musoma.  
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mara, Neema Ibamba (kushoto) akizungumza mikakati ya mkoa wa Mara katika kutekeleza Mpango wa Kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto katika kikao kilichowakutanisha kamati ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto mkoa wa Mara.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mathias Haule (kulia) akizungumza umuhimu wa uwepo wa Kamati ya Ulinzi kwa Wanawake na Watoto kwa Kamati ya Mkoa wa Mara katika kikao kilichofanyika leo mjini Musoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi kwa Wanawake na  Watoto mkoa wa Mara wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao hicho kilichofanyika mkoani humo. (PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO WAMJW)

 Na Mwandishi Wetu Mara

Mkoa wa Mara umeweka Mipango dhatiti katika kuhakikisha wanapambana na vitendo vya kikatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwa kuhakikisha wanaifikia jamii katika kutoa ujumbe sahihi wa kuaondokana na vitendo vya kikatili hasa vitendo vya ukeketaji vilivyoshamiri mkoani humo.

Hayo yamebainika leo mkoani Mara wakati wa kikoa cha wadau kutoka Kamati ya Ulinzi ya Wanawake na Watoto pamoja na wawakilishi wa Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Mara kwa lengo la kupokea jumbe mbalimbali zitakazosaidia kuelimisha jamii ya mkoa huo kuondokana na mila potofu zinozopelekea vitendo vya kikatili kwa wanawake na watoto.

Akifungua kikao hicho Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Musoma. Vicky Mbunde amesema kuwa kwa Mkoa wa Mara kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013 vitendo vya ukatili wa kijinsia vilikuwa asilimia 72 na vimepungua kufikia asilimia 66 mwaka 2015/2016.

Ameongeza kuwa tatizo la vitendo ya ukatili mkoa wa Mara sio vya kutengenzwa bali kwa kiasi kikubwa matatizo hayo husababishwa na mila potofu zinazochangiwa na uwepo wa mfumo dume ambayo inaathiri ustawi wa wanawake na watoto mkoani humo.

Vicky asema kuwa Serikali ya Mkoa wa Mara imejipanga katika kuhakikisha inatokomeza vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwemo utoaji wa elimu kwa kutumia jumbe zilizoandaliwa na mkoa kwa kutumia redio, magazeti na mikutano ili kuipa jamii uelewa wa juu ya madhara ya vitendo vya kikatili.

Ameutaja mkakati mwingine kuwa ni kampeni ya kila mwisho wa mwaka ambapo vitendo vya ukeketaji hufanyika ili kuihamasisha jamii kuachana na mila porofu zinazomgandamiza mwanamke na mtoto.

Akiwasilisha malengo ya kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati hiyo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa Clothilde Komba amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kujadiliana na kupata namna bora ya kupambana na vitendo vya ukatili mkoani humo.

Akiwasilisha jumbe katika kikao hicho Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sebastian Kitiku amesema kuwa jumbe hizo muhimu sana katika kuhakikisha jamii inabadilika na kuondokana na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages