Ligi kuu Tanzania Bara imeendelea tena leo kwa mchezo mmoja ambao umewakutanisha timu ya Lipuli FC na Singida United.
Katika mchezo huo ambao umechezwa kwenye uwanja wa Samora Iringa umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana mabao 2-2.
Mabao ya Lipuli yamefungwa na Haruna Shamte dakika ya 62 na Mirzaji Athumani (90) swakati huo huo Singida walipata mabao yao kupitia kwa Geofrey Mwashiuya (46) na Boniphace Maganga (84).
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇