LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 13, 2019

MAPROFESA 14 WA SUDAN WATIWA MBARONI

Maafisa usalama wa Sudan wameripotiwa kuwatia mbaroni maprofesa na wahadhiri 14 wa vyuo vikuu vya nchi hiyo waliokuwa wanajiandaa kushiriki katika mgomo wa kukaa kitako kama sehemu ya wimbi la maandamano ya kupinga serikali ya Rais Omar al Bashir.
Mhadhiri wa chuo kikuu, Mamdouh Mohamed Hassan ameviambia vyombo vya habari kwamba askari wa serikali ambao wamewekwa karibu na Chuo Kikuu cha Khartoum wamewatia mbaroni maprofesa 14, wanane kati yao wakiwa ni wa Chuo Kikuu cha Khartoum na sita ni kutoka vyuo vikuu vingine.
Amesema, maprofesa hao walikuwa njiani kuelekea kwenye mgomo wa kukaa ndani wakati walipozuiwa na askari wa serikali na kutiwa mbaroni.
Rais Omar al Bashir wa Sudan

Askari hao wamefunga mageti ya kuelekea kwenye eneo ambalo walalamikaji walikuwa wamekusanyika kufanya mgomo.
Picha zilizotumiwa kwenye Intaneti zinaonesha kuwa wafanya mgomo hao wamebeba mabango yenye maneno kama "Uhuru, uadilifu na amani," "Tunapinga utesaji na mauji ya waandamanaji" na nara nyinginezo.
Maandamano ya hivi sasa ya nchini Sudan ni makubwa zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha miaka 30 iliyopita. Maandamano hayo yaliyoanza kwa kulalamikia ughali wa maisha sasa yamebadilika na kuwa ni wimbi la kumtaka Rais al Bashir wa nchi hiyo ang'oke madarakani, lakini bado anashikilia msimamo wake wa kubakia uongozini.
Serikali ya Sudan imetangaza hali ya hatari katika baadhi ya mikoa ya nchi hiyo sambamba na kufunga shule na vyuo vikuu. Rais Omar al Bashir yuko madarakani nchini Sudan tangu mwaka 1993 ambapo kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, muda wa mwisho wa kubakia kwake madarakani ni mwakani yaani 2020.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages