LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 13, 2019

KIONGOZI WA MUADHAMU ATOA UJUMBE MUHIMU KWA TAIFA KUHUSU AWAMU YA PILI YA MAPINDUZI YA KIISLAMU

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo ametoa ujumbe muhimu sana kwa taifa la Iran kwa jina la "Awamu ya Pili ya Mapinduzi" kwa mnasaba wa maadhimisho ya miaka 40 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametoa ujumbe huo leo Jumatano na kusisitiza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu na taifa la Iran lina nguvu na ni imara lakini wakati huo huo lina huruma na uvumilivu bali hata ni madhlumu. Ameongeza kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hayajawahi kuwa ya kwanza kufyatua risasi hata katika kupambana na Marekani na Saddam, bali katika matukio yote, taifa la Iran na Mapinduzi ya Kiislamu yamesimama imara kujihami na kutoa majibu makali kila pale adui anapoanzisha mashambulizi.
Vile vile katika ujumbe wake huo ametaja mafanikio mbalimbali ya Mapinduzi ya Kiislamu akisema kuwa mafanikio muhimu zaidi ni pamoja na kuimarisha utulivu na usalama nchini Iran, kulinda ardhi na mipaka yote ya nchi, kuanzishwa miundombinu muhimu mno ya kiuchumi na kimaendeleo, kuongezeka kwa wingi ushiriki wa wananchi katika masuala ya kisiasa kama vile chaguzi, kuongezeka mwamko wa kisaisa wa matabaka mbalimbali ya wananchi na mtazamo wao kuhusu masuala ya kimataifa, kugawanywa kiuadilifu suhula za umma nchini, kuongezeka nembo za kimaanawi na kimaadili katika maeneo ya uma kwenye jamii na kusimama imara mbele ya njama za mabeberu na waistikbari wa dunia wakiongozwa na Marekani,
Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Aidha katika ujumbe huo Ayatullah Khamenei amebainisha kwamba mazingira yanayoikabili Iran yenye nguvu hivi sasa ni kama yaliyoikabili mwanzoni mwa Mapinduzi, yaani inakabiliwa na changamoto za kila namna kutoka kwa mabeberu. Ameongeza kuwa, kama wakati huo wa mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, mapambano na Marekani yalihusiana na kukatwa mikono na vibaraka wa maajnabi au kufungwa ubalozi wa Israel mjini Tenbran pamoja na kuvunjwa pango la kijasusi (uliokuwa ubalozi wa Marekani mjini Tehran), mapambano ya hivi sasa yanahusiana na uwepo wenye nguvu wa Iran katika mipaka ya utawala wa Kizayuni, kusambaratishwa ushawishi haramu wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi na uungaji mkono wa Jamhuri ya Kiislamu kwa mapambano ya mujahidina wa Palestina na kuhami bendera iliyopeperushwa juu ya Hizbullah na muqawama katika kona zote za eneo hili.
Vile vile kwenye ujumbe huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kisilamu ametoa nasaha katikak masuala mbalimbali kama vile elimu, utafiti, umaanawi na maadili, uchumi, uadilifu na mapambano dhidi ya ufisadi, istiqlali na uhuru, heshima ya taifa na uhusiano wa kigeni pamoja na wajibu wa kuwekwa mipaka baina ya watu humu nchini na adui na kujipamba kwa maisha mepesi na ya chini.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages