LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 25, 2019

JITIHADA ZAIDI ZIONGEZWE MIMBA ZA UTOTONI

Na Tiganya Vincent
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameshtushwa na idadi ya watoto wa kike wanaopata mimba mkoani Tabora na kuagiza hatua za kuzuia tatizo zichukuliwe.

Alisema idadi ya mimba za utotoni imengezeka kutoka 21,889 mwaka 2017 hadi mimba 27,390 mwaka 2018.

Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo juzi wilayani Kaliua katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja vya Kolimba.

Alisema kasi ya uwepo wa mimba za utotoni ni kubwa na haikubali na kutaka viongozi mkoani Tabora kubadilisha hali hiyo na kuwataka  wazazi wajitahidi kuwalinda watoto wao.

Makamu wa Rais alieleza kuwa wakati mwingine wazazi hawajitokezi kutoa ushahidi pale inapojulikana watoto wao wamepata ujauzito na kwamba na kuongeza kuwa vitendo hivyo ni kuwakatili maisha yao.

Alisema kuwa hatua za makusudi zisipochukuliwa kuna uwezekano wa kuwa na  wataalamu wa kike wachache kwa sababu ya kushindwa kutimiza ndoto zao.

Makamu wa Rais alipongeza maandamano yaliyofanywa mkoani Tabora katika kukemea na kudhibiti mimba za utotoni akisema anatambua jitihada zinazofanywa na mkoa kudhibiti hali hiyo.

Aliagiza jitihada zaidi ziongezwe kwa vile kuna ongezeko kubwa la mimba za utotoni mkoani Tabora.

Makamu wa Rais anaendelea na ziara yake Mkoani Tabora na ametembelea wilaya za Igunga,Nzega,uyui na Kaliua.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages