Algeria imeimarisha hatua za kiusalama nchini humo katika kukaribia kufanyika uchaguzi wa rais.
Askari usalama na vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo wamesambazwa kwa wingi katika maeneo ya kuingia na kutoka katika mji mkuu wa Algeria Algiers. Taarifa zinasema kuwa hatua hizo za kiusalama zimeanza kutekelezwa huko Algeria mapema sana hadi kufanyika uchaguzi wa rais huku baadhi ya jumuiya za wafanyakazi na makundi ya kiraia yakiwasilisha matakwa na malalamiko yao. Makundi ya kiraia nchini Algria juzi Jumamosi yalifanya maandamano ya amani kupinga hatua ya Rais wa sasa wa nchi hiyo Abdelaziz Buteflika ya kugombea tena kiti cha rais nchini humo.
Muungano tawala nchini humo tarehe Pili mwezi huu wa Februari ulimtangaza Rais Abdelaziz Buteflika kuwa mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama hicho. Hata hivyo vyama vinavyopinga serikali vimemtaka Rais huyo wa Algeria ajiengue katika kinyang'anyiro hicho cha uchaguzi. Buteflika amekuwa madarakani nchini Algerioa kwa mihula minne mtawalia tangu mwaka 1999. Uchaguzi wa Rais wa Algeria umepangwa kufanyika Aprili 18 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇