Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif ameashiria uamuzi wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kujiondoa rasmi katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNSECO) na kusema kitu pekee kilichobakia sasa ni kujiondoa kwao katika sayari ya dunia.
Katika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Twitter Jumanne, Zarif ameashiria mikataba kadhaa ya kimataifa ambayo rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kujiondoa ikiwa ni pamoja na mapatano ya nyuklia ya Iran maarufu kama JCPOA, Mkataba wa Biashara Huru Amerika ya Kaskazini, (NAFTA), Mkataba wa Ushirikiano wa Nchi za Pasikifi (TPP) na Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya Tabia Nchi. Zarif ameendelea kuandika kwa kuhoji, "utawala wa Trump na utawala wa Israel leo wamejiondoa rasmi UNESCO, je, kuna kingine kilichosalia kwa serikali ya Trump na utawala wake kibaraka kujiondoa? Pengine wajiondoe kwa pamoja katika sayari ya dunia!
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Oktoba 12 mwaka 2017 ilitangaza kuwa, kutokana na kuwa UNESCO ina mielekeo iliyo dhidi ya Israel, Washington itajiondoa katika shirika hilo muhimu la Umoja wa Mataifa.
Naye Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, siku hiyo hiyo aliamuru wizara ya mambo ya nje ya utawala huo kuuondoa utawala huo katika UNESCO.
Marekani ilikata misaada yake kwa UNESCO mwaka 2011 baada ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuidhinishwa kuwa mwanachama wa taasisi hiyo.
Katika azimio lake la mwezi July 2017, UNESCO ilisisitiza kuwa, Israel haina haki ya kumiliki mji wa Quds (Jerusalem). Utawala wa Kizayuni wa Israel ulikalia kwa mabavu Quds mwaka 1967. Aidha Mei 2, 2017 UNESCO ilipitisha azimio na kuulani utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kukiuka sheria za kimataifa huko Quds Tukufu na Ukanda wa Ghaza. Azimio hilo la UNESCO aidha liliitaja Israel kuwa "utawala ghasibu' .
Marekani ni muungaji mkono mkuu wa Israel katika vitendo vyake vya kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina na jinai dhidi ya watu madhulumu wa Palestina.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇