Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bi. Karolina Mtaphula akitoa hutuba yake wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kinachoendelea Mkoani Mara kuandaa ujumbe utakaotumika katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bi. Karolina Mtaphula katikati akifuatilia wakati wa kikao kazi cha kuandaa ujumbe utakaotumika katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kulia ni Bi. Grace Mwangwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii na kushoto kwake ni Bw. Edward Litunda pamoja na Bw. Emanuel Kisongo viongozi waandamizi wa Ofisi ya Mkoa wa Mara.
Baadhi ya Wajumbe wakiwa tayari kwa maandalizi ya ujumbe utakaotumika katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto leo Mkoani Mara.
Neema Ibamba Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mara akitoa maelezo wakati wa kuandaa ujumbe utakaotumika katika mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
NA ANTHONY ISHENGOMA-MARA.
JAMII mkoani Mara bado inaendeleza mila potofu ya kuamini kuwa mwanamke asiyekeketwa ni mkosi kwa familia jambo ambalo linaendeleza vitendo vya kwa ukatili wa hali ya juu dhidi ya wanawake Mkoani humo.
Akiongea wakati wa ufanguzi wa Kikao kazi cha uzinduzi wa Kampeini ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto leo Mkoani Mara Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bi. Karolina Mtaphula amesema inapotokea binti anayekeketwa akapoteza maisha kutokana na ukeketaji binti huyo amekuwa akitupwa polini bila kuzikwa kwa taratibu za kawaida kwasababu jamii pia inaamini ni mkosi kwa jamii na kwa familia yake.
Aidha Bi. Mtapula aliongeza kuwa Jamii ya Mkoa wa Mara inatakiwa ijilinganishe na mikoa mingine ambayo haina mila ya ukeketaji ili kujenga ufahamu kuwa wanawake kutoka jamii hizo kama wamekuwa wakileta mikosi katika familia zao kama amabavyo mila zao inawafanya waamini.
‘’Wanawake katika Mikoa ambayo haina ukeketaji wanazidi kupiga hatua za kimaendeleo na kufaidika kielimu lakini katika Mkoa wa Mara mila potofu imeendelea kurudisha nyuma maendeleo ya wanawake hivyo nawaomba mlinganishe na jamii hizi kuona kama kweli wanawake wasipokeketwa wanaleta mikosi’’. Alendelea kusema Bi. Mtapula.
Aidha Bi. Mtapula alisema pamoja na kuwepo kwa vitendo vaya ukatili amesema vitendo hivyo katika Mkoa wa Mara takwimu zilizopo zinaonesha vitendo vya mkoani humo vimeanza kupungua kwani kwa takwimu za mwaka 2010 mkoa huo uliongoza kitaifa kwa kuwa na sailimia 72 lakini kwa takwimu za mwaka 2015-216 takwimu zinaonesha mkoa umeshuka hadi kufikia asilimia 55.
Wakati huo huo Mkurugenzi anayeshugulikia masuala ya watoto Bw. Sebastian Kitiku amewaambia wajumbe wa kikao kazi hicho kuwa wizara iko mkoani humo kukutana na kujadiliana na viongozi wa Mkoa na Halmashauri pamoja na viongozi wadini kwa ajili kutengeneza ujumbe utakaotumika katika kampeini ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
Amewataka wajumbe hao kutengeneza ujumbea amabao kimsingi utaendana na mazingira ya Mkoa ikiwemo mila nzuri zilizopo kwakuwa ujumbe unatumika Mazingira ya Mara unaweza usitumike katika mikoa mingine kutokana na tofauti za kimazingira. Kazi ya kutengeneza ujumbe kwa ajili ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni inaendelea itaendelea katika mikoa yenye takwimu za juu katika ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambayo ni mikoa ya Shinyanga, Tabora, Singida na Rukwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇