LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 8, 2019

RAIS MAGUFULI AFANYA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI NA KUFUNGUA UBALOZI MPYA WA NCHINI CUBA

Rais Dk. John Magufuli amempandisha cheo aliyekuwa Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko kuwa waziri kamili wa madini huku Stanslaus Nyongo akimuacha kuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo.

Katika mabadiliko hayo ya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri Rais amemteua Angela Kairuki ambaye alikuwa Waziri wa Madini kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu/Uwekezaji.

Pia Rais Magufuli ameteua Makatibu Wakuu wanne na Naibu Makatibu Wakuu wawili, ili kujaza nafasi za Makatibu Wakuu waliostaafu kama ifuatavyo;
  

Joseph Nyamhanga - Katibu Mkuu TAMISEMI
Zainabu Chaula – Katibu Mkuu Afya
Elius Mwakalinga – Katibu Mkuu Ujenzi
Doroth Mwaluko – Katibu Mkuu Sera
Doroth Gwajima - Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI
Francis K Michael - Naibu Katibu Mkuu UTUMISHI

Vile vile Rais Magufuli amemteua Dkt. Mpoki Ulusubisya kuwa Balozi, ambaye kituo chake cha kufanyia kazi kitatangazwa baadaye.

Pia Rais Magufuli amefungua Ubalozi mpya wa Tanzania nchini Cuba ambao utakuwa katika mji wa Havana, na Balozi wake atatangazwa hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages